Na Neema Kandoro, Mwanza
Leo tarehe 27/6/2024, Leonard Qwihaya, ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) maarufu kama Manguzo, amehitimisha ziara yake ya siku tatu katika Jimbo la Nyamagana kwa kutoa msaada wa mifuko 720 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za chama hicho.
Qwihaya amewataka wapenzi na wakereketwa wa chama hicho kuwa mstari wa mbele katika ujenzi wa ofisi ili waweze kuwa na uhakika wa sehemu ya kufanyia kazi zao za kila siku.
Alisisitiza kuwa ujenzi wa miundombinu ni hatua muhimu katika kuimarisha uhai wa chama na hivyo kuendelea kuwa kimbilio la Watanzania wakati wote.