Home Kitaifa MIJADALA YA SERIKALI YA KUONGEZA THAMANI MADINI, YALETA TIJA KWA WACHIMBAJI NA...

MIJADALA YA SERIKALI YA KUONGEZA THAMANI MADINI, YALETA TIJA KWA WACHIMBAJI NA WAUZAJI

Na Fatma Ally Mzawa Online Media

Imeelezwa kuwa Serikali ya Tanzania inalenga kuongeza thamani madini yanayozalishwa nchini humo jambo ambalo litavutia wawekezaji wengi kutoka ndani na nje ya nchi pamoja na kuongeza thamani ya mnyororo wa madini.

Aidha mijadala ya kukutana kwa pamoja wadau wa madini kutoka ndani na nje ya nchi inalenga kutoa tija kwa jamii na wananchi kwa ujumla.

Hayo yameleezwa jijini Dar es Salaam na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Angola Gold Ashanti (GGML) Simon Shayo wakati alipokua katika maonyesho ya madini yaliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere sambamba na mkutano wa siku tatu uliolenga kujadili mada kuu ya uongezaji wa thamani madini kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa nchi ya Tanzania.

Amesema kuwa, mada ya uongezaji thamani madini ni nzuri ambayo imeleta wadau mbalimbali kuanzia wawekezaji, Serikali, wasimamizi wa sekta na watu wengine zikiwemo sekta binafsi na NGO’S ambapo lengo lim fikiwa kuanzisha mjadala mkubwa ambao unaufanya Tanzania kujiendeleza katika uongezaji wa thamani madini bila kupoteza umuhimu na nafasi yake.

Aidha, amesema kampuni Gold Ashanti wametumia fursa hiyo kuwepo na kubadilishana mawazo na wadau ambapo wameeleza tangu kuwepo kwa uongezaji thamani madini wao kama wachimbaji na wauzaji wa nje nchi yameongezeka kwa asilimia 90 ambapo wao ni wakongwe kwenye sekta ya uchimbaji wa madini .

“Leo tumeskia watu wakizungumzia suala la uchimbaji endelevu, utunzaji wa mazingira, uchimbaji wa madini unaozingatia maadili, hiyo kwetu ni ajenda kubwa sisi kama Gold Ashanti tunaliaminina tunaliishi na kutambua mchango wa mnyororo wa thamani katika uchimbaji wa madini wakiwemo, wachimbaji, wauzaji, Serikali na jamii”amesema

Ameongeza kuwa, nchi ya Tanzania Ina safari ndefu ya kuwa moja wa vinara duniani hivyo wanaendelea kutoa wito kwa Serikali kuendelea kueka mazingira yatakayovutoa wawekezaji wadogo, wakubwa, wa kati na wa nje ya nchi, lengo ni kuwa nchi indelee kuchukua nafasi na kuongeza ushindani kama moja ya maeneo yanayofaa kuekeza.

“Leo nikishiriki mada ya uchimbaji endelevu ambapo tumeeleza kama kampuni kinara wa kufanya uchimbaji endelevu Kwa kuzingatia mazingira, maendeleo endelevu Kwa jamii inayozunguka, mahusiano na wadau yanayojenga mijadala yenye tija matumizi ya nishati jadidifu”amesema

Ameongeza kuwa hakuna kampuni leo inayoweza kujinadi duniani kama inafanya uchimbaji wenye tija kama uchimbaji wake sio endelevu ambapo sisi tumekuwa mfano mzuri wa kuigwa .

Aidha, ameiomba Serikali kuwashirikisha kwenye utungaji wa sera, sheria na kanuni wadau hasa waadini wanashiriki kutoa maoni yao nini kifanyike ambapo hiyo inakua fursa, katika eneo ambalo Serikali limefanya vizuri kwa siku za hivi karibuni ni kufanya mijadala na wadau.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!