Home Burudani MBENG’O ZIMEFUNGUKA YABADILISHA MAISHA YA MUUGUZI DODOMA

MBENG’O ZIMEFUNGUKA YABADILISHA MAISHA YA MUUGUZI DODOMA

KAMPUNI ya michezo ya kubashiri nchini Betika yakabidhi rasmi zawadi ya Mshindi wa droo ya promosheni ya “Mbeng’o zitafunguka” kwa Mshindi wa Daladala Anselm Manga kutoka Mkoani Dodoma.

Akizungumza wakati wa Makabidhiano hayo Leo Septemba 08,2023 Afisa Habari wa Betika Rugambwa Juvenalius amesema Kampuni hiyo imekuwa ikiendesha promosheni mbalimbali na kuanzia mwezi Agosti ilitambulisha rasmi promosheni ya “Mbeng’o zitafunguka ” kwa miezi miwili.

Aidha, amesema droo hiyo iliweza kumpa nafasi ya kushinda zawadi ya Bodaboda na milioni 3 kila wiki na kiasi cha milioni 2.5 kwa watu watano kila siku na zawadi kubwa kabisa ya daladala mwisho wa mwezi.

Pia ametoa rai wanaocheza droo hii kuendelea kutupia ubashiri kwani zawadi ya daladala ya pili itatangazwa mwishoni mwa mwezi Septemba.

Juvenalius ameongeza kuwa Droo hizo zinazofanywa na betika zimekuwa zikibadilisha Maisha ya watanzania wengi kutokana na aina ya zawadi zinazotolewa ikiwemo fedha pamoja na vyombo vya moto sanjari na kuwaleta making mabingwa Jijini Dar es Salaam kushuhudia derby ya Simba na yanga.

Kwa upande wake Mshindi wa Promosheni hiyo ya Betika Aviator Anselim Mangu ameeleza namna alivyokuwa akitumia muda wake wa Mapumziko kufanya ubashiri na hatimae kuibuka mshindi wa daladala hiyo mpya.

“Mimi ni muuguzi hospitali ya Mkoa wa dodoma nimekuwa nikishiriki mara kwa mara mchezo huu na kwa mara ya kwanza nimewahi kushinda shilingi laki 5 nikahamasika zaidi kuendelea kutupia ubashiri mara kwa mara ili nilivopata simu kutoka uongozi wa betika sikuamini nilisubiri siku ifike niweze kuja Dar es Salaam kukabidhiwa zawadi hii ya Daladala.”

Mangu ameeleza hisia zake kwa namna amekabidhiwa daladala hiyo na kuwahahisishia watanzania kuwa hakuna janja janja ni kweli betika wanatoa zawadi .

Aidha amesema daladala hiyo itatumika kwa shughuli za usafiri Mkoa wa Dodoma kwenda kondoa kutokana na shughuli zake zaidi kuwa mikoani humo hivyo ataweza kurahisisha shughuli za usafirishaji kwa wakazi hao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!