Home Kitaifa KITENGO CHA METROLOJIA TBS KUCHOCHEA UKUAJI WA BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI

KITENGO CHA METROLOJIA TBS KUCHOCHEA UKUAJI WA BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI

 Na Mwandishi Wetu.

Wito umetolewa kwa Wawekezaji, Wafanya biashara  na Wazalishaji nchini kutumia huduma za Shirika la Viwango Tanzania (TBS), hususan katika sekta ya vipimo (metrolojia), kutokana na kutambulika kwake kimataifa.

Akizungumza na wanahabari Aprili, 2, 2026 jijini Dar-es-Salaam, Afisa Mkuu wa Metrolojia Joseph Kadenge kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) amesema kuwa Metrolojia (Sayansi ya Vipimo) ni Moja ya Misingi minne ya Ubora inayoangalia ubora wa vipimo katika mashine zinazotumika katika uzalishaji. 

Amesema ubora wa bidhaa unaanzia kwenye mashine zinazozalishia, kama mashine hazina vipimo sahihi basi hata ubora wa bidhaa uko mashakani.

Kadenge ameongeza kuwa TBS ina Maabara ya Taifa (National Metrology Laboratory) ya Vipimo inayotambulika kimataifa kupitia Shirika la Vipimo Duniani (BIPM), huku uwezo wake wa upimaji ukiwa umeorodheshwa katika kanzidata ya kimataifa.

Aidha, maabara hizo zimepata ithibati ya umahiri kutoka taasisi ya kuangalia umahili ya nchi za SADC inayoitwa SADCAS, hatua inayothibitisha ubora wa huduma zake na kuwahakikishia wawekezaji kuwa huduma za vipimo zinapatikana kwa viwango vinavyokubalika kimataifa.

Kupitia umahiri huo, Kadenge ametoa wito kwa wawekezaji na wazalishaji kutokuwa na hofu ya kuwekeza Tanzania kwani upatikanaji wa huduma ya Ugezi (Calibration) zinapatikana kwa urahisi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!