
Mjasiriamali Daniel Deogratus Sambo, mkazi wa Kigoma Mjini, ameibuka mshindi wa pikipiki aina ya TVS kupitia promosheni ya “Shinda Boda”.
Akizungumza baada ya kupokea zawadi hiyo, Sambo alisema ushindi huo utamsaidia kurahisisha shughuli zake za kila siku pamoja na kukuza biashara zake. Alieleza kuwa licha ya kushiriki kwa muda mrefu bila mafanikio makubwa, hakukata tamaa hadi alipofanikiwa kushinda pikipiki hiyo.

Katika tukio hilo, mshindi mwingine, Doreen Massawe, alisema pikipiki aliyoshinda itamsaidia katika shughuli zake za kilimo na kurahisisha usafiri wakati wa kusimamia kazi zake mashambani.
Kwa upande wake, Afisa Masoko wa PigaBet Tanzania, Hemed Msonge, alisema tukio hilo ni sehemu ya utoaji wa zawadi kwa washiriki waliobahatika katika droo.








