Home Kitaifa KAMPENI YA “JIFICHUE” YAZINDULIWA KWA AJILI YA KUTOA ELIMU YA AFYA YA...

KAMPENI YA “JIFICHUE” YAZINDULIWA KWA AJILI YA KUTOA ELIMU YA AFYA YA AKILI

Kutokana na kukithiri kwa vitendo vyenye uhusiano na masuala ya afya ya akili nchini mtanzania anayefahamika kwa jina la Belinda ameanzisha kampeni ya JIFICHUE ili kuisaidia jamii kuvunja ukimya.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Dar es Salaam leo, Belinda Nendiwe Nyapili ambaye ni Mkurugenzi wa Marcus Mwemezi Foundation amesema ameamua kuanzisha kampeni hiyo ili kuinusuru jamii.

Amesema iwapo kampeni hiyo itamfikia kila mmoja upo uwezekano wa kupunguza vitendo vya Mauaji, Ukatili na hata ubakaji maana hayo yote yana uhusiano mkubwa na afya ya akili.

Tumeanza pia kupita shuleni na kuzungumza na wanafunzi kwa lugha nyepesi kabisa juu ya afya ya akili lakini mwakani tunatarajia kwenda mbele zaidi kwa kuongeza wigo wa elimu shuleni” Belinda Nendiwe Nyapili Mkurugenzi wa Marcus Mwemezi Foundation.

Akizungumza katika uzinduzi huo wa kampeni ya “JIFICHUE” Said Kuganda ambaye ni Daktari wa Afya ya akili kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili amesema ni rahisi mtu kutambua kuwa afya yake ya akili ina changamoto na mtu anapopata mabadiliko anapaswa kupatiwa matibabu.

Mwanzo wa kukusaidia unapopata changamoto ya afya ya akili ni watu wanaokuzunguka cha msingi ni watu kuamua kufunguka juu ya hali wanazoziona zikiwakabili” Said Kuganda Daktari wa Afya ya akili.

Amesema Watoto wanapaswa kutazamwa kwa karibu katika masuala ya afya ya akili kwa kuzungumza nao.

Dk. Kuganda amesema mabadiliko ya tabia yana uhusiano mkubwa na matatizo ya afya ya akili hivyo mtu mwenyewe anaweza kujikagua na kuelewa changamoto aliyo nayo.

Mmoja wa wanawake waliowahi kukumbwa na ugonjwa wa “Sonona” aliyejitambulisha kwa jina la Angel Marry Kato ambaye pia ni mwanamuziki, amesema aliondokana na hali hiyo baada ya kuvunja ukimya.

“Tunapaswa kuwa na ukaribu na watu na kuwasikiliza pia kutopuuza mambo yanayozungumzwa na watu mfano kila siku mtu anasema atajiua ni muhimu kufuatilia nini sababu” Angel Marry Kato Aliyetaka kujiua

Najma Paul ni mtangazaji mtangazaji naa mwanzilishi wa “Kovu la Thamani” ambaye amesema ubaguzi wa watoto kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kimaumbile unaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa afya ya akili.

Mtangazaji Michael Baruti ambaye pia ni mwanaharakati wa masuala ya afya ya akili hasa kwa wanaume amesema amejikita kutazama wanaume kutokana na mazingira ya sasa kuwepo na vitendo vingi vya mauaji vinavyotekelezwa na wanaume ambavyo vinauhusiano na afya ya akili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!