Home Kitaifa KAMATI YA BUNGE  YAZIPONGEZA NDC, TBS, BRELA na TIRDO KWA UTOAJI HUDUMA...

KAMATI YA BUNGE  YAZIPONGEZA NDC, TBS, BRELA na TIRDO KWA UTOAJI HUDUMA BORA KWA WANANCHI

Kamati  ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imepongeza Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania(TIRDO) kwa utendaji kazi mzuri katika kuboresha utoaji wa huduma kwa umma kwa urahisi

Pongezi hizo zimetolewa Januari 16, 2026 Bungeni jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mhe.Deodatus Mwanyika, baada ya Taasisi hizo kuwasilishwa Taarifa ya utekelezaji wa majukumu yake katika Kikao cha Kamati hiyo

Mwanyika akiongoza Kikao cha Kamati hiyo pia alizitaka Taasisi hizo kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi katika kutoa huduma bora na kuongeza nguvu katika utoaji wa elimu kwa wananchi ili kuchochea ushindani na ukuaji wa sekta ya viwanda na biashara nchini.

Aidha, Wajumbe wa Kamati hiyo walipata fursa ya kutoa maoni na mapendekezo mbalimbali yaliyolenga kuboresha utendaji kazi wa NDC, TBS, BRELA na TIRDO ili ziweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuendelea kushughulikia changamoto zinazoibuka katika utoaji wa huduma kwa Wananchi pamoja na kusimamia Miradi ya kimkakati ya Maendeleo kwa weledi.

Naye, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga akiwa ameambatana na Naibu Waziri wake Mhe. Dennis Londo (Mb), Naibu Katibu Mkuu Dkt. Suleiman Serera, Menejimenti ya Wizara na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara yake, ameihakikishia Kamati hiyo kuwa Wizara yake itayafanyia kazi maoni na mapendekezo yote yaliyotolewa na kuahidi kushirikiana na Kamati hiyo katika kuziwezesha Taasisi hizi kutejeleza majukumu yake kwa ufanisi ili kupata Matokeo chanya yanayotarajiwa katika kuendeleza Sekta ya Viwanda na Biashara na kukuza uchumi kwa ujumla.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mwendeshaji wa NDC, Dkt. Nicolaus Shombe, alieleza kuwa Shirika hilo limepiga hatua katika usimamizi wa Miradi ya Kimkakati na kielelezo,uendekezaji wa Kongani za viwanda na uendeshaji wa Kiwanda cha Viuadudu na uzalishaji wa mbolea ya viuatilifu.

Nao Mkurugenzi Mkuu wa BRELA Bw. Godfrey Nyaisa Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt. Ashura Katunzi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Ramson Mwilangali wakiwasilisha taarifa za utekelezaji wa Majukumu ya Taasisi zao kwa Kamati hiyo walibainisha kuwa Taasisi zao zinalenga kutoa Huduma bora kwa urahisi kwa Wafanyabiashara na Wananchi kwa ujumla ili kukuza uchumi kwa ujumla.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!