Home Kitaifa CBE YATOA UJUZI WA BIASHARA NA USAFIRISHAJI, YAFUNGUA FURSA ZA AJIRA

CBE YATOA UJUZI WA BIASHARA NA USAFIRISHAJI, YAFUNGUA FURSA ZA AJIRA

Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kimeendelea kutoa mafunzo yanayolenga kuimarisha uwezo wa wajasiriamali na wataalamu wa sekta ya usafirishaji kupitia kozi fupi na za muda mrefu zinazokidhi mahitaji ya soko la ajira nchini.

Akizungumza Juni 20, 2026, katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea jijini Dodoma, Afisa Udahili Mwandamizi Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Lilian Mashalo, amesema Chuo hicho kinatoa kozi fupi kwa wajasiriamali wadogo na wa kati ili kuwajengea uwezo wa kutunza kumbukumbu za biashara, kusimamia mitaji na kuongeza tija katika shughuli zao.

Amesema Chuo hicho pia kinatoa kozi ya muda mfupi ya huduma za mabasi, ambayo imewawezesha vijana wengi wa kike na wa kiume kupata ajira katika sekta ya usafirishaji nchini.

Mashalo amesema mbali na kozi fupi, CBE hutoa programu za muda mrefu kuanzia ngazi ya cheti, diploma hadi shahada ya kwanza katika taaluma ya Transport and Logistic Management, ambayo ni miongoni mwa kozi za kimkakati zinazolenga kuandaa wataalamu wa sekta ya usafirishaji na ugavi.

Ameeleza kuwa wahitimu wengi wa programu hiyo wamepata ajira katika maeneo mbalimbali, ikiwemo mradi wa SGR, kampuni za mabasi na kampuni nyingine za usafirishaji.

Aidha, amesema wanafunzi wanaosoma kozi ya Transport and Logistic Management hupata fursa ya mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kuanzia ngazi ya cheti na diploma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!