Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amezungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti na kusaini kwenye kitabu cha wageni cha Mkoa wa Mtwara katika Makao makuu ya Mkoa huo. Leo Julai 29, 2022.
Waziri Bashungwa alikuwa safarini kuelekea Mkoani Lindi katika ziara ya kikazi ambapo leo atamwakikisha Mheshimiwa Rais katika hafla ya kumpongeza mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya kusukuma maendeleo vijijini na mjini nchi nzima iliyoandaliwa na mkoa wa Lindi.
Pamoja na hayo, wamejadili mambo mbalimbli ikiwa ni pamoja na Mkoa ulivyojipanga vyema kuwafikishia viuatilifu vya Salfa wakulima wa korosho pia kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ndani ya Mkoa wa Mtwara.