Home Kitaifa BASHUNGWA ATOA MAAGIZO KUHUSU MALALAMIKO YA WANANCHI KATIKA STENDI WA MAGUFULI DAR...

BASHUNGWA ATOA MAAGIZO KUHUSU MALALAMIKO YA WANANCHI KATIKA STENDI WA MAGUFULI DAR ES SALAAM

Na OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla kukutana na wadau na wamiliki wa mabasi ili kuweka utaratibu mzuri ambao ni shirikishi wa utoaji huduma kwa wananchi kwenye kituo kikuu cha mabasi cha Magufuli Dar es salaam.

Bashugwa ametoa maelekezo hayo leo Agosti, 30, 2022 wakati akitoa ufafanuzi kuhusu malalamiko ya utoaji wa huduma kwa wananchi wanaoingia Mkoa wa Dar es salaam kupitia kituo kikuu cha Mabasi cha magufuli.

Bashungwa amesema amekuwa akifuatilia kwa Ukaribu Malalamiko yanayotolewa na wananchi Kuhusu huduma zinazotolewa katika stendi ya Magufuli kwa abiria wanaoingia na kutoka katika mkoa wa Dar es salaam ambayo yanatafisiri vibaya malengo ya Serikali ya Kutenga bilioni 50 kujenga stendi hiyo.

Kuna abiria wanaoingia mkoa Dar es salaam na kushushwa katika stendi ya Magufuli lakini wanahitaji mabasi hayo yawafikishe mjini kwenye vituo vya mabasi vilivyojengwa na sekta binafsi, kwahiyo Mkuu wa Mkoa akikuta na wadau hao wataona namna nzuri ya kusimamia suala hilo” amesema Bashungwa

Aidha, Bashungwa amemtaka Mkuu wa Mkoa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) pamoja na wadau wengine ili kukubaliana na kuweka utaratibu utakaorahisisha utoaji wa huduma bora bila kuleta adha kwa wananchi wala kuadhiri malengo ya Serikali kujenga stendi hiyo.

Amesema Serikali inaweza kutimiza maelengo na Kusudi la Uwepo wa Stendi ya Magufuli bila kuwapa adha wananchi wanaolazimika kushushwa katika stendi na kuingia Kwenye gharama za kutafuta usafiri mwingine wa kuwafikisha mjini wakati yapo mabasi yanaweza kupita katika stendi na yakaendelea na safari ya kuwafikisha abiria Mjini.

Pia, Amefafanua kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi na kuendelea kuimarisha usalama wa wananchi na Wageni wanaoingia nchini kwa kutumia usafiri wa magari kwa kuwatambua kupitia stendi hiyo ambayo kuna idara ya Uhamiaji na vyombo vingine vya usalama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!