Na Shomari Binda-Musoma
MASHINDANO ya “Mathayo Cup” yanayoandaliwa na mbunge wa jimbo la Musoma mjini,Vedastus Mathayo,yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi agosti 28.
Mwenyekiti wa kamati ya mashindano hayo,Meya wa manispaa ya Musoma, Patrick Gumbo amesema maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri.
Amesema tayari wameshakutana na viongozi kutoka Kata zote 16 zitakazoshiriki mashindano hayo na kupanga taratibu na kanuni za kuendesha mashindano hayo.
Gumbo amesema moja ya taratbu zilizopangwa ni kila timu kuhakikisha zinafanya usajili mapema wa wachezaji itakaowatumia.
Amesema mashindano ya mwaka huu yatakuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila Kata kuonekakana kujiandaa vizuri na mashindano hayo.
“Tumekutana na viongozi wa timu shiriki na kukubaliana masuala mbalimbali ya kuendesha mashindano yetu ya mwaka huu”
“Tunamshukuru mheshimiwa Mathayo kwa kuendelea kuhamasisha michezo jimboni kila mwaka na mwaka huu zawadi zimeboreshwa zaidi” amesema Gumbo.
Amesema agodti 27 mashindano hayo yatafunguliwa kwa mchezo wa ufunguzi kati ya timu za mashabiki wa Simba na Yanga.
Tayari makundi 4 yamepangwa ambapo kundi A mechi zake zitakazochezwa uwanja wa Posta lina timu za Mukendo,Mwigobero,Iringo na Kitaji..
Kundi B michezo yake itakayochezea uwanja wa Buhare itakuwa na itakuwa na timu za Makoko, Mwisenge, Buhare na Kamnyonge.
Kundi C uwanja wa Mara sekondari ina timu za Kigera, Nyamatare, Kwangwa na Nyashu huku kundi D zitakazochwzewa uwanja wa Musoma sekondari kitakuwa na timu za Nyakato, Mshikamano, Rwamlimi na Bweri.








