Home Kitaifa SHIVYAWATA WAIPONGEZA SERIKALI KWA JINSI INAVYOENDELEA KUWATAMBUA WATU WENYE ULEMAVU

SHIVYAWATA WAIPONGEZA SERIKALI KWA JINSI INAVYOENDELEA KUWATAMBUA WATU WENYE ULEMAVU

Na Theophilida Felician, Kagera

Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu SHIVYAWATA Halmashauri ya Bukoba Mkoani Kagera kupitia Mwenyekiti wake Jackline Phabiani ametoa pongezi na kuishukuru Serikali kwa namna inavyozidi kulitambua kwa ukaribu kundi la watu wenye ulemavu nyanja tofauti tofauti.

Mwenyekiti huyo ameyabainisha hayo kwenye mkutano wa kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa shirikisho hilo uliofanyika ofisi za Halmashauri.

Amesema kuwa kwa sasa Serikali imekuwa ikitumia juhudi nyingi katika kuyatengeneza mazingira rafiki kwa malengo ya kulipa kipaumbele kundi hilo kupitia fursa kadha wa kadha hususani suala la kupunguza makali ya mikopo kwa kundi hilo.

Amefafanua kuwa hapo nyumba masharti ya kupata mkopo kwa kundi la watu wenye ulemavu moja wapo lilikuwa la kujiunda kundi la watu watano watano ili wapate mkopo tofauti na sasa kigezo hicho kimepunguzwa hivyo hata kwa mtu mmoja ataweza kupata mkopo huo.

“Mimi naishukuru sana Serikali chini ya Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kwakututambua watu wenye ulemavu kwasababu imetoa fursa ya mikopo kwa watu wenye ulemavu ilianza kuhitaji kundi la watu watano watano ila sasa imeluhusu kwa mtu mmoja mmoja baada yakuona Mazingira yao ni tofauti kuungana mpaka wakarejesha kama kundi ni changamoto tunaendelea kuomba Serikali kupunguza masharti lakini si masharti ya kuipoteza hela ya Serikali badala yake ni masharti ya kumpunguzia mizunguko huyu mtu mwenye ulemavu anapokwenda kwa awamu ya kwanza kuwasilisha ombi lake basi kwa muda mfupi aweze kupata pesa aliyoihitaji na aweze kuanza mradi wake mara moja, chamsingi wale wanaotoa mkopo kuhakikisha wanajiridhisha na ule mradi wa mtu mwenye ulemavu ikiwa nipamoja na kuamini kabisa kwamba anaenda kurejesha mkopo huo kwa uaminifu”. ameeleza kwa undani Mwenyekiti Jackline

Ameelendelea kutoa ufafanuzi akisema kuwa kutokana na juhudi hizo za Serikali kuwatambua nakuwathamini nao wamejipanga kuhakikisha wanasimama kidete katika kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kuleta maendeleo kiuchumi.

Ameongeza kuwa watu wenye ulemavu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto hasa zakupata vifaa ambavyo nivitendea kazi pale wanapokuwa na malengo yakunzisha mradi jambo ambalo limekuwa kikwazo cha kuwakwamisha nakushindwa kusonga mbele kimaendeleo.

Ametoa wito kwa watu wenye ulemavu wanaoenda kuomba mikopo serikalini kuhakikisha wanapata dhamana ya Serikali za mitaa wanakotokea ili iwasaidie kufahamika vizuri nakuweza kupata mikopo kwa urahisi.

Katika uchaguzi huo Jackline Phabiani amekabidhiwa kiti hicho kwa mara yangine tena baada ya muda wa miaka mitano kuisha, ambapo Nestory Shumbusi Karist amechaguliwa kuwa Katibu na Ajuwaye Anthony amechaguliwa kuwa mweka hazina.

Katibu wa chama hicho Nestor Shumbusi akisoma taarifa ya shirikisho hilo amebainisha kuwa wanachangamoto za hapa na pale ikiwemo ya kutokuwa na ofisi yakuendeshea shughuli zao ngazi ya wilaya.

Kwa upande wake Afisa ustawi wa jamii Joyce Chibalula akiwa ameshiriki mkutano huo kwaniaba ya Mkurugenzi amewaahidi kuwa Serikali inaendelea kutoa ushirikiano wakutosha kwa shirikisho hilo kama yalivyomatakwa ya Serikali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!