Na Shomari Binda-Musoma
MAELFU ya wakazi wa mji wa Musoma mkoani Mara, miji jirani na nje ya nchi wamehudhuria mazishi ya kada wa CCM na mfanyabiashara,Magori Zembwela.
Miongoni mwa waliohudhuria ni wakuu wa mikoa mitatu wakiongozwa na mkuu wa Mkoa wa Mara Said Mtanda, Mkuu wa Mkoa wa Njombe na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Yahaya Nawanda.
Licha wakuu hao wa mikoa, mazishi ya kada huyo aliyefariki agosti 12/kwenye hospital ya Taifa Muhimbili ni pamoja na wabunge wa mkoa wa Mara na mkuu wa jeshi la polisi nchini( IGP) Camilius Wambura.
Wakitoa salamu za rambirambi kwa nyakati tofauti viongozi hao wamemzungumzi kada huyo na kusema ni mtu tofauti aliyekuwa na mchango mkubwa kwa jamii.

Wamesema Magori ni mmoja wa vijana ambaye amekuwa akisaidia jamii kwenye uchangiaji wa masuala mbalimbali huku jamii ikiombwa kuiga mfano wake.
Mkuu wa mkoa wa Njombe, Antony Mtaka amemuelezea alivyomfahamu Magori tangu walipokuwa wakisoma shule ya sekondari Mwembeni kwa namna alivyokuwa na moyo wa upendo.
Mtaka amesema ameamua kutumia muda mfupi kuja kumsinfikiza Magori kutokana na moyo wa upendo aliokuwa nao.
Mbunge kutoka nchini Kenya jimbo la Kurya West Mathias Robbi amesema Magori ni moja ya watu wazuri kama walivyo watanzania ambao siku zote wamekuwa wakalimu.
Amesema amemfahamu Magori kutokana na kutaka maendeleo bila ubinafsi na kuwa na hamu ya kumsaidia kila mmoja enzi ya uhai wake.
Mkuu wa mkoa wa Mara, Said Mtanda amewashukuru wale wote waliohudhuria mazishi ya kada huyo na ushitikiano walioutoa wa wafiwa na wananchi wa Musoma na mkoa wa Mara.
Kwa mujibu ws historia ya marehemu iliyosomwa na wadogo zake imeeleza kuwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na moyo na amefariki akiwa na umri wa miaka 42.









