Home Kitaifa TPA YAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA UWEKEZAJI WA BANDARI ZA ZIWA VICTORIA

TPA YAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA UWEKEZAJI WA BANDARI ZA ZIWA VICTORIA

Celebrating 25 Years of NHIF

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uwekezaji wa zaidi ya Shilingi bilioni 60 katika kuboresha bandari za Mwanza Kaskazini, Bukoba na Kemondo, hatua inayolenga kuimarisha usafirishaji wa abiria na mizigo, kurahisisha biashara na kuchochea ukuaji wa uchumi katika Ukanda wa Ziwa Victoria.

Shukrani hizo zimetolewa jijini Mwanza na Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria, Rosemary Ndesamburo, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa, ambaye amesema uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuimarisha miundombinu ya usafiri wa majini na kuongeza fursa za kiuchumi kwa wananchi.

FAHARI AFYA

Ndesamburo amesema maboresho ya Bandari ya Mwanza Kaskazini yalianza Mei 2023 kwa gharama ya Shilingi bilioni 18.6 na hadi sasa yamefikia asilimia 83, huku yakitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2026,ameeleza kuwa maboresho ya Bandari za Bukoba na Kemondo yamekamilika kwa asilimia 100.

Amesema uwekezaji huo una manufaa kwa wananchi na wafanyabiashara wa Ukanda wa Ziwa Victoria kwa kurahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo, kuimarisha biashara na kufungua fursa zaidi za kiuchumi,aidha, TPA imeahidi kuendelea kusimamia na kutunza miundombinu hiyo ili kuongeza ufanisi wa huduma za bandari.

Kwa upande wao, baadhi ya abiria wanaotumia Bandari ya Mwanza Kaskazini wamesema maboresho hayo yameongeza ubora wa huduma, hususan upatikanaji wa maeneo mazuri ya kupumzikia na kusubiri safari,wamesema hali hiyo imeboresha mazingira ya kusubiri usafiri na kuwafanya wafurahie zaidi huduma za usafiri wa majini.

Uwekezaji huo unatarajiwa kuendelea kuimarisha nafasi ya bandari za Ziwa Victoria katika kurahisisha biashara na usafirishaji wa bidhaa, hivyo kuongeza mchango wa sekta ya usafiri wa majini katika uchumi wa ukanda huo na taifa kwa ujumla.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!