Home Kitaifa DKT. MWIGULU ATEMBELEA NA KUKAGUA TAASISI YA ELIMU YA USHIRIKA NA BIASHARA...

DKT. MWIGULU ATEMBELEA NA KUKAGUA TAASISI YA ELIMU YA USHIRIKA NA BIASHARA KIZUMBI

Celebrating 25 Years of NHIF

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo (Jumatatu, Novemba 9, 2026), ametembelea na kukagua Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB), Manispaa ya Shinyanga, ikiwemo jengo la taaluma na bweni la wanafunzi wa kike yaliyojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 8.98.

Majengo hayo yamejengwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.

FAHARI AFYA

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu ametembelea madarasa, kuzungumza na wanafunzi na kuwahimiza kujituma katika masomo.

Awali, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema Serikali inaendelea kupanua fursa za elimu ya juu katika Kanda ya Ziwa kupitia ujenzi wa vyuo na kampasi katika mikoa mbalimbali.

Amesema uwekezaji uliofanyika Kizumbi ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa HEET nchini, huku akitambua mchango wa Dkt. Mwigulu katika upatikanaji wa fedha za mradi huo alipokuwa Waziri wa Fedha.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), Anna S. Makinda, ameishukuru Serikali kwa uwekezaji huo, akisema umeboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika taasisi hiyo.

Akiwasilisha taarifa ya mradi, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, Prof. Alfred S. Sife, amesema majengo hayo tayari yanatumika na yamepunguza changamoto ya uhaba wa nafasi za kufundishia, kujifunzia na malazi.

Amesema uwekezaji huo umeongeza uwezo wa taasisi kupokea wanafunzi kutoka 1,201 mwaka 2021 hadi 2,967 mwaka 2026, huku nafasi za malazi zikiongezeka kutoka 242 hadi 454.

Prof. Sife amesema jengo la taaluma lina kumbi za mihadhara, vyumba vya semina, maabara ya kompyuta, ofisi za watumishi na eneo la kukuza ubunifu wa biashara.

Ameongeza kuwa bweni jipya lina uwezo wa kuchukua wanafunzi wa kike 212, huku usanifu wake ukiruhusu kuongezwa kwa ghorofa katika hatua zinazofuata. Aidha, michoro ya bweni la wanafunzi wa kiume tayari imeandaliwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!