Mkurugenzi wa Upasuaji wa Ubongo MOI Dkt. Lemeri Mchome amesema leo Septemba 17, 2026 kuwa technolojia hiyo ni ya kwanza kutumika nchini na kwamba inakwenda kuleta mapinduzi katika matibabu ya kiharusi.
“Tunatoboa tundu ndogo kichwani na tunapitisha kifaa maalum chenye kamera, Ile kamera inakwenda kutuonyesha eneo ambalo damu imevilia na kutuwezesha kuitoa bila kuathiri sehemu nyingine” amesema Dkt. Lemeri
“Hii ndiyo teknolojia ya kisasa zaidi duniani na sisi kama taasisi hatuko nyuma, wagonjwa wa kiharusi hawana sababu ya kukimbilia nje ya nchi Kwa matibabu, huduma hiyo inapatikana MOI…kwasasa tunapokea wagonjwa watatu hadi watano Kwa siku, teknolojia hii inakuwa msaada wa matibabu bora” ameongeza
Naye Daktari bingwa wa Upasuaji wa Ubongo MOI, Dkt. John Mtei ambaye ameshiriki katika upasuaji wa kwanza kwa kutumia kifaa hicho amesema technolojia hiyo inaacha alama katika mapinduzi ya tiba ya Kiharusi nchini.
“Ufanisi wa matibabu ndiyo nyenzo muhimu katika matumizi ya technolojia hii, mgonjwa anafanyiwa upasuaji na kuondolewa tatizo lake kwa uhakika” amesema Dkt. Mtei
Taasisi ya MOI imeendelea kujikita katika kuleta afua mbalimbali hapa nchini za kuipunguzia Serikali mzigo wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa rufaa za gharama kubwa na pia kuendelea kuwa kituo cha weledi cha matibabu ya Mifupa na mfumo wa fahamu barani Afrika.

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imeanza kutumia technolojia ya kisasa kutoa matibabu ya kibingwa ya upasuaji wa ubongo kwa wagonjwa wa kiharusi inayongeza ufanisi wa matibabu Kwa wagonjwa.