Home Kitaifa UTAZIPENDA SIMU HIZI MPYA KUTOKA YAS NA ZTE , WAWEZA KUNUNUA AU...

UTAZIPENDA SIMU HIZI MPYA KUTOKA YAS NA ZTE , WAWEZA KUNUNUA AU KUKOPA KWA BEI NAFUU SANA.

Na Adery Masta.

Dar es Salaam – 26 Septemba 2025: Katika jitihada za kuongeza upatikanaji wa simu za mkononi na kukuza matumizi ya huduma za kidijitali nchini Tanzania, kampuni inayoongoza kwa huduma za kidijitali, Yas, ikishirikiana na ZTE, imezindua rasmi simu mpya aina ZTE Blade A36 na ZTE Blade A76.

Simu hizi mpya zinachukua nafasi ya matoleo ya awali, ZTE A35 na A75, zilizozinduliwa mwaka 2024 na kuwa chachu ya upatikanaji wa teknolojia ya simu nchini. Matoleo mapya yanakuja na kamera zilizoboreshwa, utendaji ulioimarishwa, na chaguzi rahisi za ununuzi, zikilenga kufanya teknolojia ya kisasa ya simu iweze kufikiwa na mamilioni ya Watanzania.

Kupitia ushirikiano huu, simu hizo zitapatikana kwenye maduka yote ya Yas kote nchini kwa njia ya malipo ya fedha taslimu au kupitia mpango wa malipo ya mkopo. Wateja watakaotumia mpango wa mkopo wanaweza kulipa ndani ya miezi 6 au 12, malipo ya chini yakiwa Tsh. 700 kwa siku, ikiambatana na bando la masaa 24 kila siku. Wateja wa malipo ya fedha taslimu watapata bando la kwa mwaka mzima.

Imelda Edward, Meneja wa Vifaa na Huduma za Intaneti wa Yas, alisema:

“Kupitia ushirikiano wetu na ZTE kuleta Blade A36 na A76 sokoni, tunawawezesha Watanzania kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali, kupata huduma muhimu, na kuungana na dunia. Simu hizi ni hatua nyingine ya dhamira yetu ya kubadilisha maisha ya Watanzania kupitia teknolojia.”

Naye Bw. Duan Cunxin, Meneja Mkaazi wa ZTE, alisema:

“Tanzania ni soko linalokua kwa kasi lenye fursa kubwa za mabadiliko ya kidijitali. Kupitia ushirikiano huu na Yas, tunazindua simu zinazounganisha bei na utendaji, kuhakikisha Watanzania wengi wanaweza kufurahia maudhui mitandaoni na huduma za kidijitali.”

Uzinduzi huu unafuatia ongezeko la mahitaji ya intaneti ya simu nchini, ambayo tayari yameongezeka kwa asilimia 36.75%. Simu hizi, zenye bei ya chini na kati, zinatarajiwa kushindana sokoni kutokana na ofa za mikopo ya kipekee ambayo haipatikani kwa watoa huduma wengine.

Kwa mpango huu, Yas na ZTE wanajiweka mstari wa mbele katika mapinduzi ya simu za mkononi nchini, wakilenga kuunganisha Watanzania wengi zaidi, kuhamasisha matumizi ya data, na kuendeleza mtindo wa maisha ya kidijitali kwa wote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!