Home Kitaifa ZAIDI YA WANANCHI 1,500 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJIKO BANIFU WILAYANI BABATI

ZAIDI YA WANANCHI 1,500 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJIKO BANIFU WILAYANI BABATI

Mkuu wa Wilaya ya wa Babati, Mheshimiwa Emmanuela Kaganda, leo Novemba 12, 2025 kwa niaba ya wakazi wa wilaya ya babati amezindua mradi wa uuzaji na usambazaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku.

Uzinduzi huu ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya mkuu wa mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga akiwataka wakuu wa wilaya wote wa mkoa wa manyara kuzindua na kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku katika wilaya zao.

Uzinduzi umefanyika katika kata ya Magugu wilayani babati, ambapo jumla ya majiko banifu 1,582 yatauzwa na kusambazwa kwa bei ya ruzuku ya TZS 11,200 ambayo ni sawa na aslimia 80 ya ruzuku ya TZS 56,000 ambayo ni bei ya awali ya jiko.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mheshimiwa Kaganda amesema mpango huo umelenga kuhakikisha wananchi wote, hususani wa kipato cha chini, wanapata fursa ya kutumia nishati safi na salama ya kupikia kwa gharama nafuu.

Aidha, amewataka wananchi kuacha kutumia nishati zisizo salama za kupikia na kuanza kutumia nishati safi na salama ili kulinda afya zao na mazingira.

“Kampeni hii si tu inalenga kuboresha afya za wananchi, bali inalenga kulinda mazingira kwa kupunguza uharibifu wa misitu unaotakana na matumizi makubwa ya mkaa na kuni” amesema Kaganda.

Mpango huu wa ruzuku unatarajiwa kuongeza upatikanaji wa nishati safi , salama na nafuu ya kupikia kwa wananchi na hivyo kuwa chachu ya mabadiliko kuelekea upishi salama na rafiki kwa mazingira.

Akiwasilisha taarifa ya mradi kwa kwa wakazi wa babati waliojitokeza katika uzinduzi huo, Mhandisi wa miradi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini, Ramadhani Mganga amesema,

Kwa wilaya ya babati mradi unatarajia kusambaza na kuuza majiko 1,582 na kila jiko kuuzwa kwa bei ya ruzuku ya TZS 11,200 tu.

Mhandisi Mganga amesema, ili mwananachi aweze kununua jiko atatakiwa kuwa na kitambulisho cha taifa (NIDA) au namba ya kitambulisho cha taifa ambayo ataambatanisha na kitambulisho cha mpiga kura au udereva na pesa taslimu TZS 11,200 tu.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!