Home Michezo Yanga Yavunja Mkataba na Kocha Romain Folz

Yanga Yavunja Mkataba na Kocha Romain Folz

Klabu ya Young Africans SC imetangaza rasmi kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Romain Folz, kuanzia Oktoba 18, 2025. Uamuzi huo umefikiwa kwa makubaliano ya pande zote mbili baada ya tathmini ya kiufundi ndani ya benchi la ufundi la timu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Young Africans SC, uongozi wa klabu hiyo umemshukuru Kocha Folz kwa mchango wake katika kipindi alichokuwa akiongoza kikosi hicho na kumtakia mafanikio katika majukumu yake mengine ya baadaye. Klabu imesisitiza kuwa inatambua kazi nzuri aliyoifanya katika kuendeleza kikosi na kuleta ushindani kwenye mashindano mbalimbali.

Wakati mchakato wa kumpata Kocha Mkuu mpya ukiendelea, majukumu ya kuiongoza timu yamekabidhiwa kwa Kocha Msaidizi Patrick Mabedi ambaye ataongoza benchi la ufundi kwa muda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!