
Klabu ya Yanga SC imeanza vibaya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL) baada ya kukubali kichapo cha bao 1–0 kutoka kwa wenyeji wao, Silver Strikers ya Malawi, katika mchezo uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Bingu National Stadium jijini Lilongwe.
Licha ya kuonesha mchezo mzuri katika kipindi cha pili, Yanga walishindwa kuipenya ngome ya wapinzani wao waliocheza kwa nidhamu ya hali ya juu na kutumia vizuri nafasi chache walizopata.

Bao pekee la Silver Strikers lilifungwa kipindi cha pili na kuamsha shangwe kwa mashabiki wa nyumbani. Yanga sasa wanalazimika kushinda kwa mabao zaidi ya moja katika mchezo wa marudiano utakaopigwa jijini Dar es Salaam wiki ijayo ili kufuzu hatua inayofuata.