Home Kitaifa WMA MARA YALIDHISHWA NA MATUMIZI YA MIZANI MASOKONI

WMA MARA YALIDHISHWA NA MATUMIZI YA MIZANI MASOKONI

Na Shomari Binda-Butiama

WAKALA wa vipimo mkoa wa Mara (WMA) imeonyesha kulidhishwa na matumizi ya vipimo vinavyotumika kwenye uuzaji wa bidhaa mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Meneja wa WMA mkoa wa Mara, Muhoni Nashon wakati akitoa elimu juu ya matumizi ya vipimo katika mnada wa soko la Butiama ikiwa ni maadhimisho ya siku ya vipimo duniani.

Amesema wakala wa vipimo mkoa wa Mara wakati wa utekelezaji wa majukumu ya kila siku wa ukaguzi wa mizani wanalidhishwa na matumizi yake.

Muhoni amesema matumizi sahihi ya vipimo vya bidhaa zikiwemo za vyakula yana umuhimu mkubwa ndio maana wamejikita katika utoaji wa elimu.

Amesema wauzaji na wanunuzi wakipata elimu ya matumizi sahihi ya vipimo kutakuwa na uelewa mpana na kutakuwa hakuna udanganyifu.

Kila tarehe 20 mei ya kila mwaka ni siku ya vipimo duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema ” Vipimo katika kuwezesha mfumo wa usambazaji wa chakula duniani” tumeitumia siku hii kutoa elimu.

Kwa mkoa wa Mara hali ya matumizi ya vipimo ni nzuri kurokana na elimu ambayo imeendelea kutolewa lakini kwa wale wanaokutwa na makosa ya kuchezea mizani wanatozwa faini”,amesema Muhoni.

Kaimu Meneja huyo amewataka wafanyabiashara na wale wanaotumia vipimo kufika ofisi za vipimo pale wanapoona changamoto yoyote ya vipimo wanavyotumia.

Wananchi walioshuhudia zoezi hilo la utoaji elimu wa (WMA) wamesema imewasaidia kujua umuhimu wa vipimo kwa watoa huduma na wanaohudumiwa.

Mmoja wa wananchi hao mkazi wa Butiama aliyejitambulisha kwa jina la Maria Warioba,amesema yeye kama mnunuzi ameomba zoezi la elimu na ukaguzi liwe endelevu kwa manufaa ya wote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!