Na Magreth Mbinga
Watumishi wa umma wametakiwa kutambua nafasi zao sababu watu wengi wapo nje wanatamani nafasi hizo kwa kujituma kwa moyo mmoja watafanya vizuri .
Hayo yamezungumzwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh Deogratius Ndejembi katika kikao chake na watumishi wa Manispaa ya Temeke ambacho kimelenga kusikiliza na kutatua changamoto ambazo walikuwa nazo.

Pia Mh Ndejembi amesema Watumishi wa Umma lazima watambue miiko ya Utumishi kwa kuifahamu na kuiishi,watambue maadili katika Utumishi.
“Unaweza kuta Watumishi wanafanya kazi kwa mazoea mpaka wanasahu uwajibikaji, mahusiano mazuri ,usiri katika maeneo ya kazi ndugu zangu narudia tena tujitambue“amesema Ndejembi.

Aidha Mkurugenzi Manispaa ya Temeke Mh Elihuruma Mabelya amemshukuru Naibu Waziri na kusema kuwa wamepokea maagizo ambayo amewapatia ya kushughulikia malimbikizo ya mishahara na madeni ya watumishi ambayo hayajashughulikiwa kwa muda mrefu.
“Tunaomba utufikishie salamu kwa Mh Rais kwamba Watumishi wa Manispaa ya Temeke tunaunga mkono juhudi zake na tutafanya kazi usiku na mchana“amesema Mh Mabelya.

Sanjari na hayo Afisa afya mazingira Idara ya Afya kitengo cha udhibiti wa taka na usafi wa mazingira Jane Ndongo amesema wataendelea kufanya kazi na kutatua changamoto zote kwa kujituma kufanya kazi kwa hiyari kwakuwa wameomba kazi niwajibu wao kutekeleza.








