Home Kitaifa WATUHUMIWA 69 WA MAKOSA MBALIMBALI WAKAMATWA MKOANI TANGA

WATUHUMIWA 69 WA MAKOSA MBALIMBALI WAKAMATWA MKOANI TANGA

Na Boniface Gideon, TANGA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linaendelea kutekeleza majukumu yake ya kulinda usalama wa raia na mali zao, ambapo katika kipindi cha hivi karibuni limefanya misako na operesheni mbalimbali na kufanikiwa kukamata, kuzuia na kutanzua uhalifu, na jumla ya watuhumiwa 69 wamekamatwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Tanga.

Katika operesheni hiyo, watuhumiwa mbalimbali wamekamatwa kwa makosa ya fujo, wizi, uvunjaji wa nyumba, uporaji wa simu, udanganyifu kupitia mitandao pamoja na makosa ya dawa za kulevya na pombe bandia, ambapo hatua za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi yao.

Aidha, katika operesheni hiyo, mtuhumiwa (01) Athuman S/O Ramadhani (52) amekamatwa akiwa na katoni 46 za pombe bandia aina ya “Good Life” pamoja na vifaa vya kughushi.

Pia, watuhumiwa (02) wamekamatwa kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya aina ya bangi na mirungi.

Aidha, watuhumiwa (09) wamekamatwa kwa kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia mtandao ujulikanao kama Q-NET, ambapo wameshafikishwa mahakamani na mashauri yao yanaendelea.

Vilevile, Jeshi la Polisi linawashikilia watuhumiwa (16) maarufu kama vishandu kwa makosa ya uporaji wa simu na wizi, ambapo wamekamatwa wakiwa na pikipiki (26), kati ya hizo (18) hazina namba za usajili na (04) zimethibitika kuwa za wizi.

Aidha, katika operesheni za kupambana na dawa za kulevya, jumla ya watuhumiwa (26) wamekamatwa katika kipindi cha Machi hadi Aprili 2026.

Kwa upande wa kikosi cha Usalama Barabarani, jumla ya madereva 911 walikamatwa kwa kuvunja sheria za usalama barabarani na kupewa adhabu mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!