Na Shomari Binda-Serengeti
WANAWAKE wametakiwa kusemea kazi nzuri inayofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwahudumia wananchi hususani kwenye huduma za kijamii.
Kauli hiyo imetolewa na Mjumbe wa Baraza Kuu la Wanawake wa Tanzania (UWT) Taifa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa mkoa wa Mara Robhi Samwelly kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Serengeti.
Kwenye mkutano huo wa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara Patrick Chandi wa kufatilia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho amesema ipo miradi mikubwa ambayo mefanywa na inapaswa kusemewa.
Amesema kwa kuanza na elimu Rais Samia amefanya kazi kubwa na leo hakuna anayeangaika kuhusu kuchangia ujenzi wa madarasa.
Rhobhi amesema majengo ya kisasa ya madarasa yamejengwa nchi nzima ambayo yamewawezesha wanafunzi kupata mahala sahihi pa kupata elimu.
Amesema licha ya madarasa madawati na viti vya kukalia vimepelekwa mashuleni na adha ya michango imeondoka kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Rais Samia.
Kwenye sekta ya maji Mjumbe huyo wa Baraza Kuu amesema miradi mikubwa imefanyika na kwa mkoa wa Mara mama ameendelea kutuliwa ndoo kichwani kwa miradi mingi kufanyika.
“Wanawake tunapaswa kumsemea Rais Samia kutokana na mambo mengi mazuri anayoyafanya kwa watanzania kupitia miradi mbalimbali”
“Kwenye elimu,afya,maji miundombinu kote kwa muda mfupi amefika tutembee kifua mbele na naamini ataendelea kufanya makubwa zaidi kwa wa watanzania” amesema Robhi.








