Home Kitaifa WANANCHI MUSOMA WAMTUMA MBUNGE MATHAYO KWA RAIS SAMIA

WANANCHI MUSOMA WAMTUMA MBUNGE MATHAYO KWA RAIS SAMIA

Na Shomari Binda-Musoma

WANANCHI wa jimbo la Musoma mjini wamemtuma mbunge wao kumfikishia shukrani Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan, salamu za shukrani kutokana na miradi anayowafikishia.

Ujumbe wa kufikishiwa aalama hizo wameutoa kwenye mkutano wa hadhara wa mbunge huyo uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Nyakato.

Wamesema kwa jimbo la Musoma mjini ipo miradi ambayo imewafikia ikiwemo ya afya,elimu,maji na miundombinu ambayo ina manufaa kwao na haina budi kutoa shukrani.

Kuhusu afya wamesema ujenzi wa kituo cha afya Rwamlimi unaendelea huku kituo cha afya Makoko kikiwa kimekamilika na kusaidia up at ikan ski wa huduma karibu jambo ambalo limewasaidia.

Kwenye upande wa elimu wamesema ujenzi wa madarasa mapya kwenye shule yamejengwa na kuepusha wanafunzi kubanana kama ilivyokuwa zamani.

Baadhi ya wananchi hao wamesema licha ya salamu za shukrani kwa Rais zipo changamoto nyingine ikiwe ucheleweshaji wa fedha za Tasaf kwa walengwa inabidi wapatiwe kwa wakati.

Akizungumza kwenye mkutano huo ambao ilihudhiliwa pia na viongozi wa CCM wilaya ya Musoma,mbunge Vedastus Mathayo,amesema kama mwakilishi wao atafikisha salamu hizo.

Amesema amekuwa akifikisha na kufatilia kile wananchi wanachokihitaji na yapo mengi ambayo utekelezaji wake umefanyika.

Mathayo amesema kwa sekta ya maji kwa jimbo la Musoma mjini sio sjida tena na kwa sasa ni mabomba kupasuka kwa msukumo wa maji.

Mbunge huyo amesema hiki ni kipindi cha bajeti bungeni lakini ameomba ruhusa kuja kuwasikiliza wananchi na kile walichokieleza atakiwasilisha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!