Home Kitaifa ‎WAFANYAKAZI WA TUME YA TAIFA YA MIPANGO WATAKIWA KUWA WABUNIFU NA WELEDI

‎WAFANYAKAZI WA TUME YA TAIFA YA MIPANGO WATAKIWA KUWA WABUNIFU NA WELEDI

Katibu Mkuu-Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango Dkt Tausi M. Kida ametoa wito kwa watendaji wa Tume hiyo kufanya kazi kwa weledi, ubunifu na ushirikiano ili kuishi dhana ya kufanya kazi isivyokawaida ili kuyafikia matarajio ya Taifa jumuishi, lenye ustawi, haki na linalojitegemea.

‎Dkt Kida ametoa wito huo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Mipango.

Aidha, amesisitiza ‎kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inayo matarajio makubwa kwa Tume ya kuhakikisha inatekeleza ipasavyo majukumu yake kwa weledi, ari na kuzingatia utu.

‎Mkutano huo, umeongozwa na kauli mbiu isemayo: Utumishi Imara ni Msingi wa Utekelezaji wa Dira 2050.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!