Na Magreth Mbinga
Vikundi vinne vya Kata ya Mikocheni Manispaa ya Kinondoni leo April 23 vimepata mkopo wa zaidi ya Milioni mia moja na sitini ikiwa ni muendelezo wa kuwezesha vikundi vidogo vidogo kupitia mikopo ya Halmashauri maarufu kama mkopo wa Mama Samia.

Akizungumza na wanufaika wa mkopo huo Diwani wa Kata ya Mikocheni Mhandisi Nzenzely Hussein amewataka kutumia pesa hizo kadiri ya maombi yao ambayo walitumia kuomba mkopo huo ili waweze kurejesha vizuri na wengine waweze kupata .
“Mkopo huu muende kufanya biashara kama mulivyoainisha katika fomu za maombi wenye gari mununue,bajaji pia pamoja na mama lishe nitapita kuangalia kama mumetekeleza mulichokiainisha kule”amesema Mhandisi Nzenzely.

Pia Afisa maendeleo ya jamii Kata ya Mikocheni Mwanahija Masudi amesema pesa ambazo zimepata vikundi hivyo itawezesha kujikwamua kiuchumi sababu kabla ya kuwapatia mkopo huo walipatiwa elimu juu ya kuendesha Kikundi,kutengeneza katiba na naman ya kutumia pesa hizo ili ziweze kuwa na manufaa kwao.
“Mkopo huu ni nafuu kabisa kwanza hauna riba nia njema ya Mh Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ni kuwakwamua katika hali ngumu ya maisha hivyo mukafanyie biashara pesa hizo muweze kurejesha kwa wakati na wengine waweze kupata mkopo huo kurejesha kwenu vizuri ndio mlango wa wengine kunufaika na mkopo huo”amesema Mwanahija.
Aidha Mwenyekiti wa Kikundi cha vijana kilichosajiliwa kwa jina la CHAMABAVI Ndugu Salumu Shedwad amesema wao kama Kikundi wamepatiwa mkopo wa Milioni mia moja ishirini na tano .
CHAMABAVI tumepatiwa mkopo wa Shilingi Milioni mia moja ishirini na tano kwaajili ya kununua gari ya abiria aina ya TATA ambayo itafanya biashara ili kuweza kupata marejesho gari hiyo itakuwa na Bima tupo katika taratibu za mwisho za kupata njia lakini utaratibu es kupata gari umeshakamilika”amesema Shedwad









