Home Kitaifa UMIKIDO WASHIRIKI MKUTANO MKUU WA MWAKA WA VYOMBO VYA UTANGAZAJI

UMIKIDO WASHIRIKI MKUTANO MKUU WA MWAKA WA VYOMBO VYA UTANGAZAJI

Umoja wa Vyombo vya Habari vya Mitandao ya Kijamii Mkoa wa Dodoma (UMIKIDO) umeshiriki Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji nchini.

Mkutano huo wa siku mbili unafanyika katika Ukumbi wa New Generation jijini Dodoma, ukianza leo Februari 12, 2026. Mkutano huo umeandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Katika mkutano huo, mada na mafunzo mbalimbali yanawasilishwa kwa waandishi wa habari pamoja na wadau wa sekta ya utangazaji.

Aidha, kunafanyika mijadala mbalimbali inayolenga kujadili masuala muhimu yanayohusu maendeleo na uboreshaji wa vyombo vya utangazaji nchini.

Mkutano huo umefunguliwa rasmi na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!