
Ujumbe kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Zanzibar, Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI na Benki ya Dunia upo nchini Rwanda kwa ziara ya kujifunza mbinu shirikishi zinazotumiwa na jamii ya Nchi hiyo kwa ngazi ya familia katika kupambana na ukatili.

Ujumbe huo unaongozwa na Bi. Abeida Rashid Katibu Mkuu- Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, (Zanzibar) ambapo leo hii wamekutana na kujitambulisha
Ubalozi wa Tanzania nchini humo. Ugeni huo umepokelewa na Mhe. Dkt. Habibu Kambanga- Balozi wa Tanzania nchini Rwanda.

Wengine waliombatana na ujumbe huo ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Felister Mdemu, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia Badru Abdunuru, Mkurugenzi wa Sera Mipango, Victor Nkya na Waratibu wa Mradi wa PAMOJA kutoka Wizara hizo.








