Kampuni ya Serikali Twiga Minerals Corporation, yenye ubia na kampuni ya kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Barrick Gold Corporation, ni mdhamini mkuu wa mkutano wa Jukwaa la Pili la utekelezaji wa ushirikishwaji Watanzania katika sekta ya madini.
Mkutano huu unaofanyika kila mwaka umeandaliwa na Serikali kupitia Tume ya Madini chini ya Wizara ya Madini na unafanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha International Conference Centre (AICC), na kukutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta hiyo ya madini kwa lengo la kujadili na kufanya tathmini ya ushirikishwaji watanzania katika mnyororo wa sekta hiyo.
Waziri wa Madini, Mh. Dkt. Doto Biteko, anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mkutano huo kesho.
Mkutano huo wenye kauli mbiu ya “Ushirikishwaji wa Watanzania katika sekta ya madini kwa kufungamana na sekta nyingine kwa uchumi imara wa nchi” unaambatana na maonyesho ya makampuni mbalimbali yanayojihusisha na shughuli za uchimbaji wa madini nchini.








