
Na Magrethy Katengu — Dar es Salaam
KAMPUNI ya TripBey imekuja na mfumo wa huduma za usafiri unaowawezesha wananchi kusafiri kwa ndege, mabasi na treni bila kulipa nauli kabla ya kuanza safari, hatua inayolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za usafiri nchini Tanzania na katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Kupitia huduma hiyo, watumiaji wanaweza kuomba tiketi za usafiri kwa kutumia programu ya simu ya TripBey na kulipa gharama za safari baadaye, kulingana na masharti na vigezo vilivyowekwa na mtoa huduma.
Akizungumza Jijini Dar es salaam Oktoba 14 wakati wa uzinduzi wa Mfumo huo Afisa Masoko Mwendeshaji Trip bey Idrisa Njeru amesema App hiyo imeunganishwa na inakwenda kuwapa wananchi unafuu katika kupanga safari zao, hususan wale wanaohitaji kusafiri kwa dharura au ambao hawana fedha za keshi za kulipia nauli mara moja.
Katika utekelezaji wa huduma hiyo, TripBey inatumia mfumo wa tathmini ya uwezo wa kifedha wa mtumiaji (Ability to Pay) ili kubaini kama ana uwezo wa kulipa gharama za safari baada ya kupata huduma.
Tathmini hiyo inalenga kuhakikisha kuwa watumiaji wanaopata fursa ya kusafiri kwa utaratibu huo wanakidhi vigezo vya kifedha vilivyowekwa, huku wakizingatia masharti ya ulipaji wa nauli baada ya safari.
“Huduma hii inajumuisha aina mbalimbali za usafiri, zikiwemo ndege za ndani, mabasi ya mikoa na treni,pikipiki, jambo linaloweza kuwapa wananchi chaguo pana zaidi la kupanga safari zao kulingana na mahitaji yao.
Naye Balozi wa Kampuni hiyo Maulid Kitengu amesema Sasa mtu kukosa kwenda Mikoni na safari za hapa ndani ya Dar es salaam kisingizio cha kukosa nauli Badi kinachotakiwa kudawlod App ya trip bey ukiwa na simu janja utapata kusafiri popote na utalipia baadae
Aidha Kitenge amesema kupitia matumizi ya teknolojia ya kidijitali, TripBay inalenga kurahisisha mchakato wa kupata tiketi na kutoa mfumo mbadala wa malipo ya usafiri unaowawezesha watumiaji kupata huduma kwanza na kulipa baadaye.
Aidha wananchi wanaotaka kutumia huduma hiyo wanashauriwa kufahamu masharti ya malipo, vigezo vya kustahiki na gharama zinazoweza kuhusishwa na huduma hiyo kabla ya kufanya maombi ya tiketi.









