Home Kitaifa TAKA ZA VIFAA VYA KIELETRONIKI ZAZIDI KUONGEZEKA NA KUWA TATIZO KIMAZINGIRA

TAKA ZA VIFAA VYA KIELETRONIKI ZAZIDI KUONGEZEKA NA KUWA TATIZO KIMAZINGIRA

Na Magrethy Katengu

Licha ya kuwepo na Udhibiti wa takataka Ili kupunguza uharibifu wa mazingira imeelezwa kuwa Wimbi wa taka zinazotokana na matumizi ya Teknolojia zimezidi kuongezeka siku na kuwa tishio la bado halijapata ufumbuzi namba ya kuzigeuza kuwa fursa

Akizungumza Leo Jijini Dar es salaam Waziri wa Habari Mawasiliano Teknolojia ya habari n Nape Nauye Wakati akifungua Warsha ya tano ya Uhamasishaji wa Usimamizi taka za Kielektroniki kwa Ukanda wa Afrika Mashariki(EACO) ambapo amesema kutokana na Teknolojia inavyozidi kukua na watu kununua vifaa hivyo imeonekana kuwa baada ya miaka kadhaa vifaa hivyo vikifa hutupwa holela hivyo kupitia warsha hiyo ya Leo iangaliwe namna ya vifaa hivyo vikifa vikusanywe na kugeuzwa fursa ili visizagae mazingira.

“Taka zinazotokana na vifaa vya elekroniki Sasa limekuwa tatizo na limeendelea kukua siku hadi siku watu Wanaweza wasione Kwa haraka matokeo yake kwani na watu wanatupa popote vifaa vingine vinaweza kuwa sumu na vikaleta madhara kwa Jamii hivyo kupitia Mkutano huu utakaofanyika kwa siku tatu utaleta suluhisho namna Bora ya kuzikusanya taka hizi na kuzigeuza fursa ili kudhibiti uharibifu wa Mazingira” amesema Waziri

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano ya TCRA Dkt Jabiri Bakari amesema kuwa Leo warsha hiyo watajadili namna ya kufanyia kazi tafiti zilizofanyika kuhusu taka za Kielektroniki hivyo tumekusanyika Wadaumbali kujadiliana namna Bora ya kudhibiti taka hizo.

“Taka hizo zinazidi kuongezeka kwani vipo vifaa vinavyokuja vipya vilivyoisha muda wake,feki ,vilivyokufa, hivyo TCRA mwezi wa tano tutaanza mkatakati wa kuhakikisha kabla vifaa hivyo havijaja nchini kule vinakotokea tunavikagua” amesema Mkurugenzi

Mkurugenzi Mkuu TCRA amesema mpaka Sasa hawana takwimu sahihi za hizo taka za Kielektroniki lakini hivyo kuna baadhi ya Kampuni na taasisi chache zimeanza kukusanya taka hizo na tutahakikisha tunashirikiana nao na kuwapatia utaratibu mzuri Ili wasizifukie kwani zinaleta shida kimazingira

Kwa Upande Katibu Mamlaka ya Mawasiliano Jumuiya Ukanda wa Afrika Mashariki EACO Dkt Ally Simba amesema wameangalia kwa Ukanda huu wa Afrika Mashariki na ikanekana kuwa kuwa taka za vifaa vya Kielektroniki zinakuwa kwa kasi zaidi kuliko taka nyingine hivyo hivyo lazima tuweke mikakati ya pamoja kuweza kudhibiti taka hizo

“Takwimu zinaonesha takribani watu Bilioni 7 Duniani wanatumia vifaa vya kielektoniki hivyo vinapokufa hawana hutupwa hivyo na kuzagaa hivyo kupitia warsha hii tumeona vifaa vya Kielektroniki si tatizo isipokuwa inatakiwa mikakati taka hizo kugeuzwa kuwa fursa wa kuzichakata kama taka nyingine” amesema Dkt Simba

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!