Home Kitaifa SIKA: NITASHANGAA KUONA MTU ANAPANGA FOLENI ILI KUPIGIA KURA UPINZANI KISARAWE

SIKA: NITASHANGAA KUONA MTU ANAPANGA FOLENI ILI KUPIGIA KURA UPINZANI KISARAWE

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe, Ndugu Shabani Sika, leo Ijumaa Septemba 26, 2025, amehutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika Viwanja vya Kisarawe Sokoni na kuwataka wakazi wa Kisarawe kuhakikisha wanakipa kura nyingi chama hicho ifikapo Oktoba 29, 2025.

Akihimiza mshikamano wa wana Kisarawe, Sika amewataka wapiga kura kumpa kura ya ndiyo Mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisema Rais huyo ana mapenzi makubwa kwa Kisarawe na tayari amepeleka fedha nyingi kutekeleza miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo.

Dkt. Samia amethibitisha kuthamini Kisarawe, maana kati ya wabunge 372 amemuona Mbunge wetu Dkt. Selemani Jafo na kumpa nafasi ya uwaziri. Hii ni heshima kubwa kwetu kama Kisarawe,” alisema.

Aidha, amewaomba wananchi wa Kisarawe kumpa kura Dkt. Jafo ili aendelee na kazi kubwa ya maendeleo aliyofanya kwa bidii kubwa usiku na mchana.

Pia amewaomba wakazi wa kata ya Kisarawe kumpa kura mgombea udiwani wa CCM, Abel Samwel Mudo, akisema ni kiongozi asiyechoka kushughulikia matatizo ya wananchi.

Kata ya Kisarawe ina wapiga kura 5,578. Nitashangaa sana kuona mtu anapanga foleni ya kupiga kura chama cha upinzani. Tumeshuhudia mengi yamefanyika Kisarawe, ni wajibu wetu kukipa kura chama kilichotuletea maendeleo,” alisema.

Sika amesisitiza kuwa wapiga kura wa Kisarawe wanapaswa kuendeleza imani yao kwa CCM ili kufanikisha maendeleo zaidi yanayoendelea kuletwa na serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!