Home Kitaifa SERIKALI YAONDOA URASIMU KUKUZA UWEKEZAJI VIWANDA VYA DAWA

SERIKALI YAONDOA URASIMU KUKUZA UWEKEZAJI VIWANDA VYA DAWA

Serikali ya Tanzania imetangaza kuondoa urasimu ili kuharakisha uwekezaji katika viwanda vya dawa nchini kupitia mkakati mpya wa kuhimiza maendeleo ya sekta hiyo ya kimkakati.

Akizungumza leo Januari 19, 2026 jijini Dar es Salaam katika Jukwaa la Uwekezaji wa Viwanda vya Dawa Tanzania, Waziri wa Afya Mohamed Mchengerwa amesema sekta ya dawa ni muhimu kwa afya, uchumi na usalama wa taifa, hivyo haiwezi kuendelea kufuata taratibu ndefu za maamuzi.

Amesema serikali imeanzisha mfumo wa haraka wa kushughulikia masuala ya uwekezaji ili kuondoa vikwazo vya kimfumo, ambapo utoaji wa leseni, vibali, ardhi, kodi, usajili wa bidhaa na miundombinu vitashughulikiwa kwa pamoja kwa wakati mmoja badala ya kufuatana hatua kwa hatua.

Aidha, Waziri Mchengerwa amesema serikali imeunda Kikosi Kazi cha Kuharakisha Uwekezaji wa Dawa (PIAT) chenye mamlaka ya kuratibu na kuharakisha uwekezaji wa kimkakati kuanzia tathmini hadi utekelezaji wa mwisho, kikihusisha watoa maamuzi kutoka sekta zote muhimu kwa mtazamo wa kitaifa.

Amesisitiza kuwa PIAT haitahusika tu na kutoa maamuzi bali pia itafuatilia utekelezaji wa miradi kwa wakati ili kuhakikisha Tanzania inafikia lengo la kuwa kitovu cha uzalishaji wa dawa Afrika na duniani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!