Home Kitaifa SERIKALI INATHAMINI MCHANGO WA MZEE MKALI-RAIS SAMIA

SERIKALI INATHAMINI MCHANGO WA MZEE MKALI-RAIS SAMIA

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kuenzi na kuthamini mchango wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Wazee mkoa wa Dar es Salaam, Mzee Hemedi Bakari Mkali kwa kujitoa kwake kwa maslahi ya Taifa tangu enzi za kupigania Uhuru.

Hayo yamesemwa leo (Ijumaa Julai 14, 2023) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipomwakilisha Rais Dkt. Samia katika mazishi ya Mzee Mkali yaliyofanyika Kiluvya Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mamia ya waombolezaji, Mheshimiwa Majaliwa amewataka Watanzania kuenzi yote mazuri aliyoyafanya Mzee Mkali enzi za uhai wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!