Home Kitaifa REA YAENDELEA KUTEKELEZA KWA VITENDO MKAKATI WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA .

REA YAENDELEA KUTEKELEZA KWA VITENDO MKAKATI WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA .

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Olivanus Thomas akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka leo Oktoba 20,2025 amezindua rasmi mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku mkoa wa Njombe. uzinduzi huo umeongozwa na mkuu wa wilaya , Maafisa kutoka REA pamoja na viongozi wengine wa mkoa, wilaya, kata, vijiji na vitongoji vyake.

Mhe. Olivanus amesema , lengo la uzinduzi wa mradi huu ni kuutambulisha rasmi mradi kwa wananchi wa mkoa wa Njombe ambao ndio walengwa na wanufaika wa mradi.

Mhe. Olivanus, amepongeza juhudi za Serikali na REA katika kufanikisha utekelezaji wa mradi na kuongeza kuwa lengo la Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia ni kuwa ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia, jambo ambalo litasaidia kutunza Afya na kuhifadhi mazingira.

Serikali imeweka ruzuku ya asilimia 85, kwa hiyo wakina Baba na kina Mama wa mkoa wa Njombe wajiandae kutumia majiko banifu,, kwetu sisi Mradi huu ni neema”. Alisema, Mhe. Olivanus.

Akiwasilisha taarifa ya mradi mbele ya Mkuu wa wilaya na wananchi waliohudhuria uzinduzi huo, Mhandisi wa miradi Kutoka wakala wa Nishati Vijijini, David Malima, amesema,

Mradi huu umekuja kwa lengo la kuimarisha na kuboresha Afya za wananchi, Mazingira, kukuza upatikanaji wa Nishati Safi na Endelevu, kupanua usambazaji wa nishati mbadala katika maeneo ya Vijijini na zaidi kuhamasisha matumizi ya teknolojia safi kupikia , teknolojia za kisasa na bora za kupikia

Mradi huu unatarajia kugharimu kiasi cha zaidi ya TZS Milioni 285.3 kwa mkoa wa Njombe pekee na utafanikisha uuzaji na usambazaji wa majiko banifu 4,836.

Uuzaji na usambazaji wa majiko banifu utafanyika katika wilaya nne (4) za mkoa wa Njombe ambazo ni wilaya ya Njombe, Ludewa, wanging’ombe na wilaya ya Makete ambapo kila wilaya majiko banifu 1,209 yatasambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku.

Mikataba ya mradi huu ilisainiwa tarehe 25 Julai, 2025 kati ya REA na mtoa huduma kampuni ya Envotec Services Limited.

Mtoa huduma atasambaza na kuuza majiko banifu kwa bei ya ruzuku katika wilaya zote nne. Gharama ya jiko moja ni TZS 59,000 lakini serikali imetoa ruzuku ya asilimia 85 sawa na TZS 50,150 hivyo mwananchi atanunua kwa gharama ya TZS 8,850 tu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!