Home Kitaifa RC MARA ATOA UJUMBE MZITO SWALA YA EID EL FITR

RC MARA ATOA UJUMBE MZITO SWALA YA EID EL FITR

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa mkoa wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mzee ameitaka jamii kuepukana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.

Licha ya kujihusisha na masyala ya ukatili kwa wanawake na watoto lakini amekemea pia vitendo vya ushoga kwa vijana kwa kuwa ni kinyume cha maadili.

Akizungumza kwenye Msikiti mkuu wa Ijumaa
mjini Musoma,amesema vitendo vya ukatili vimekithiri kwenye jamii hivyo vinapaswa kupingwa na kila mmoja.

Amesema kumekuwa na manyanyaso na ukatili kwa wanawake na watoto kwenye jamii jambo ambalo linaacha vilema na hata vifo kwa wahanga.

Mkuu huyo wa mkoa amesema jamii ikibadilika na kumuogopa Mwenyezi Mungu hakutakuwa na vitendo vya ukatili.

Akizungumzia vitendo vya ushoga kwa vijana amesema maadili yameshuka hivyo ni jukumu la kila mmoja kutenga muda wa kuzungumza na vijana na kupaza sauti kukemea ushoga.

Amesema kila mmoja asimame kukemea vitendo hivyo kwa kuwa vimekatazwa hata kwenye vitabu vya dini.

Aidha katika swala hiyo ya Eid mkuu huyo wa mkoa wa Mara amechangia mifuko 80 ya saruji na shilingi milioni 1 kwaajili ya ujenzi wa msikiti unaoendelea.

Kwa upande wake shekh wa mkoa wa Mara hasim Msabaha amewataka waislam na jamii kuzingatia ujumbe uliotolewa na mkuu wa mkoa juu ya maadili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!