
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewateua wabunge wapya sita wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mamlaka aliyo nayo chini ya Ibara ya 66(1)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Walioteuliwa ni Dkt. Dorothy Onesphoro Gwajima, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, Bw. Abdullah Ali Mwinyi, Balozi Khamis Mussa Omar, na Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho.
Taarifa hii imetolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, ikisainiwa na Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi, tarehe 10 Novemba 2025.









