Home Kitaifa RAIS SAMIA AMTEUA DKT. MWIGULU NCHEMBA KUWA WAZIRI MKUU

RAIS SAMIA AMTEUA DKT. MWIGULU NCHEMBA KUWA WAZIRI MKUU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Uteuzi huo umewasilishwa leo tarehe 13 Novemba 2025 katika Bunge la 13, Kikao cha Tatu, kinachofanyika jijini Dodoma. Hati ya uteuzi imepelekwa Bungeni na Mpambe na Mshauri wa Masuala ya Kijeshi wa Rais, Brigedia Jenerali Nyamburi Mashauri, ikiwa ndani ya bahasha maalum ambayo ilifunguliwa na Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu.

Baada ya kuifungua, Spika aliwasomea wabunge yaliyomo kwenye hati hiyo na kulitaja jina la Dkt. Mwigulu Nchemba, Mbunge wa Iramba Magharibi na aliyewahi kuhudumu kama Waziri wa Fedha katika awamu iliyopita, kuwa ndiye aliyependekezwa kushika nafasi ya Waziri Mkuu.

Hatua inayofuata ni kwa wabunge kupiga kura ili kumthibitisha kupitia Azimio litakalowasilishwa Bungeni kwa mujibu wa taratibu za kibunge.
#MzawaUPDATE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!