Home Kitaifa PETROLI DAR SASA 3,820 KWA LITA

PETROLI DAR SASA 3,820 KWA LITA

Bei ya mafuta ya petroli imepanda kwa kiwango kikubwa, ambapo katika Jiji la Dar es Salaam imeongezeka kutoka shilingi 2,864 kwa lita mwezi Machi hadi kufikia shilingi 3,820 kwa lita mwezi Aprili 2026, kulingana na taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

Ongezeko hilo linaonesha kupanda kwa shilingi 956, ikiwa ni kiwango cha juu kuwahi kushuhudiwa katika siku za hivi karibuni.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa kupanda kwa bei kunatokana na mabadiliko ya soko la kimataifa, likiwemo ongezeko la bei ya mafuta ghafi na changamoto za usafirishaji.

Aidha, hali ya kisiasa na kiusalama duniani, hususan mvutano unaoendelea kati ya mataifa mbalimbali, imechangia kuvuruga upatikanaji na usambazaji wa mafuta katika masoko ya kimataifa.

Kwa mujibu wa EWURA, gharama za uagizaji na usafirishaji zimeongezeka, zikichangiwa pia na kupanda kwa gharama za bima ya meli pamoja na ucheleweshaji wa mizigo.

Hali hii imepelekea bei za rejareja kupanda katika mikoa mbalimbali, ikiwemo Dar es Salaam, Tanga na Mtwara, ambapo bei mpya zimeanza kutumika rasmi kuanzia leo, Aprili Mosi, mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!