
Muuzaji wa mishikaki jijini Dar es Salaam, Bakari Hamisi Bakari, ameshinda boda boda katika droo ya kwanza ya kampeni ya #ShindaBoda inayoendeshwa na PigaBet, ushindi anaosema umemsaidia kuongeza kipato na kuimarisha mtaji wa biashara yake.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo, Bakari amesema chombo hicho kimemwezesha kuunganisha biashara yake ya sasa na huduma za usafiri, hatua anayoamini imeimarisha shughuli zake za kiuchumi. Amesema ushindi huo umekuwa mwanzo wa safari ya kujikwamua kimaisha na kujenga mustakabali bora.
Katika hafla hiyo, mshindi mwingine wa droo hiyo, Chirag Narsana, pia amepokea boda boda yake na amesema imerahisisha shughuli zake za kila siku na matumizi binafsi.
Kwa upande wa waandaaji, wamesema kampeni ya “Shinda Boda – Kuwa Boss Kila Wiki” imelenga kutoa fursa kwa Watanzania kujiongezea kipato huku wakisisitiza umuhimu wa kucheza kwa uwajibikaji kwa kuzingatia umri wa miaka 18 na kuendelea.








