Na Shomari Binda
MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Mara, Ghati Zephania Chomete, ameiomba serikali kupeleka miradi ya maji mashuleni ili kuweza kuwahudumia wanafunzi.
Miradi hiyo ameomba ifike kwenye shule za msingi na sekondari mkoani Mara ili kupunguza adha ya maji kwa wanafunzi.
Katika swali lake la msingi bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwenye Ofisi ya Rais TAMISEMI mbunge huyo alitaka kujua in lini serikali itapeleka miradi ya maji mashuleni ili kuwafikia wanafunzi.
Amesema maji ni moja ya huduma muhimu ambayo wanafunzi pia wanastshili kuipata kwa uhakika wanapokuwa shuleni.
” Mheshimiwa Spika nashukuru kwa majibu ya Naibu Waziri, napenda kuuliza swali la nyongeza, Je, ni lini serikali itapeleka miradi hii ili kuwasaidia wanafunzi wa mkoa wa Mara?
Akijibu maswali ya mbunge huyo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Deogratius Ndejembi amesema huduma ya maji ni muhimu na serikali ipo tayari kuifikisha hadi mashuleni.
Amesema ipo miradi ya SRWSS amvayo inaendelea ambayo itafika hadi kwenye shule za mkoa wa Mara kuweza kuwahudumia wanafunzi.
“Nikushukuru mheshimiwa Ghat Zephania Chomete kwa swali lako, maji ni muhimu na serikali ipo tayari kufikisha huduma hiyo ya maji na ipo miradi ikiwemo ya SRWSS inayoendelea”, amesema Ndejemb.








