

Mabaki ya mwili wa kijana Joshua Mollel, aliyeuawa nchini Israel na wapiganaji wa Hamas tarehe 7 Oktoba 2023, yamewasili leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Katika mapokezi hayo, Ujumbe wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa, akiwa pamoja na Balozi Silima Haji Kombo, ulihudhuria kupokea mabaki hayo.
Mabaki ya mwili wa Joshua Mollel yanatarajiwa kuzikwa kesho, tarehe 20 Novemba 2025, katika mtaa wa Njiro, Kata ya Orkesumet, Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara.









