
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt Hashil Abdallah amesema lengo la Serikali ya awamu ya Sita ni kuweka mazingira mazuri na wezeshi kwa ajili yakuendeleza Viwanda na Ufanyaji biashara Nchini ili kuleta ushindani katika bidhaa na masoko
Ameyasema hayo Disemba 12, 2023 Jijini Dar es Salaam akiwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Shirikisho la wenye Viwanda Nchini.

Dkt.Abdallah amesema kazi ya Serikali ni kulinda Usalama, ubora na uhalisia wa bidhaa na salama kwa matumizi ya binadamu pamoja na kuhakikisha bidhaa bandia kutoingia katika masoko pamoja na kushirikiana na Tume ya Ushindani (FCC) kwa pamoja kufanya uhamasishaji kwa umma juu ya athari za utumiaji wa bidhaa bandia.
Aidha Dkt Abdallah amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na Shirikisho la Viwanda Tanzania katika kudhibiti bidhaa bandia na kuweka mazingira mazuri kwa wenye Viwanda na wafanyabiashara nchini

Vilevile ametoa rai kwa wafanyabiashara na wenye viwanda nchini kuhakikisha kuwa wanalenga kuzalisha bidhaa za hali ya juu na halisi na kuwa mstari wa mbele katika kupambana na bidhaa bandia
Naye Mkurugenzi wa kudhibiti bidhaa bandia Nchini Bi. Khadija Ngasongwa kutoka FCC Naye amesema kuna umuhimu wa taasisi za Serikali kushirikiana kuibua wafanyabiashara wenye mbinu potofu katika viwanda, uchumi na maendeleo ya nchi wanaojihusisha na bidhaa zisizo halali huleta athari katika biashara na uchumi wa nchi
Naye Mwenyeki wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI) Bw. Leodga Tenga amesema watakua mstari wa mbele katika kutoa taarifa kuhusu bidhaa bandia na amehimiza wafanyabiasha wafanye usajiri bidhaa zao ili ziwezwe kutofautishwa kutoka kwenye bandia na zile ambazo ni halali.








