
Na Deborah Lemmubi-Dodoma.
Waziri wa Madini Mhe Anthony Mavunde ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2024/25 Wizara ya Madini imeyatambua na kuyapa hadhi ya vituo vya ununuzi jumla ya maeneo 142 yanayotumika kufanyia biashara ya Madini kwa wingi kupitia Gazeti la Serikali Na.906 ya tarehe 15 Novemba 2024.
Mhe Mavunde ameyaeleza hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari leo hii Mei 15,2025 Jijini Dodoma akielezea Mafanikio ya Wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia.

“Tangu kuanzishwa kwa masoko ya madini mwaka 2019, Masoko na Vituo vya Ununuzi vimeongezeka kutoka 42 na 100 mwaka 2020/2021 hadi kufikia 43 na 109 mwaka 2024/2025 mtawalia. Aidha, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Wizara imeyatambua na kuyapa hadhi ya vituo vya ununuzi jumla ya maeneo 142 yanayotumika kufanyia biashara ya madini kwa wingi (bulk minerals) kupitia Gazeti la Serikali Na. 906 ya tarehe 15 Novemba, 2024“.
Aidha amesema mchango wa Sekta ya Madini katika fedha za kigeni kwa mauzo ya bidhaa nje ya nchi umeendelea kuimarika kutoka Dola za Kimarekani Bilioni 3.1 sawa na asilimia 45.9 mwaka 2021 hadi Dola za Marekani bilioni 3.55 sawa na asilimia 46.1 mwaka 2023 huku mauzo ya bidhaa zisizo asili umeongezeka kutoka asilimia 53.8 mwaka 2021 hadi asilimia 56.2 mwaka 2023.
“Mbali ya sekta hii kuchangia mapato ya yatokanayo ni maduhuli ya Serikali, Mchango wa Sekta ya Madini katika fedha za kigeni kwa mauzo yote ya bidhaa nje ya nchi umeendelea kuimarika kutoka Dola za Marekani bilioni 3.1 sawa na asilimia 45.9 mwaka 2021 hadi Dola za Mareka.bilioni 3.55 sawa na asilimia 46.1 mwaka 2023. Aidha, kwa upande wa mauzo ya bidhaa zisizo asilia (non-traditional goods), mchango wa sekta ya madini umeongezeka kutoka asilimia 53.8 mwaka 2021 hadi asilimia 56.2 mwaka 2023″.
Moja ya kazi ya Wizara hii ya Madini ni pamoja na Kusimamia na kudhibiti biashara ya Madini na Uendeshaji wa Madini nyumba zote za Vito.








