Home Kitaifa HAMIDU: VIJANA WENZANGU MKIMCHAGUA DKT. SAMIA UJUE UMECHAGUA AJIRA

HAMIDU: VIJANA WENZANGU MKIMCHAGUA DKT. SAMIA UJUE UMECHAGUA AJIRA

Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Juma Seif Kwangaya, leo Ijumaa Septemba 26, 2025, amehutubia wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika Viwanja vya Kisarawe Sokoni na kuwasihi vijana kuhakikisha wanachagua wagombea wa CCM katika uchaguzi mkuu ujao.

Kwangaya amewaomba wananchi kumpa kura ya ndiyo Mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Dkt. Selemani Jafo, Mgombea ubunge wa Jimbo la Kisarawe, na Abel Mudo, Mgombea udiwani kata ya Kisarawe.

Tunamuombea kura Dkt. Samia kutokana na dhamira yake njema ya kuijenga nchi, ikiwemo Kisarawe. Namuombea kura Dkt. Jafo kwa sababu amekuwa kielelezo kikubwa cha kazi nzuri za kitaifa na ndani ya Kisarawe. Namuombea kura Abel Mudo kwa kuwa ni mzoefu wa kazi ya udiwani na ni mwalimu ndani ya halmashauri yetu,” alisema.

Akiwaeleza vijana, Hamidu amesisitiza kuwa ilani ya CCM imejikita kwenye kutatua changamoto za ajira.

Amesema kuanzia mwaka 2025 hadi 2030, ajira milioni nane zitazalishwa, ambapo milioni nne zitakuwa rasmi na milioni nne zisizo rasmi.

Hivyo vijana wenzangu, unapomchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan ujue umechagua ajira. Unapomchagua Dkt. Jafo maana yake umechagua maendeleo ndani ya Kisarawe, na unapomchagua Abel Mudo maana yake umechagua maendeleo ndani ya kata ya Kisarawe,” alisisitiza.

Kwangaya amehitimisha kwa kusema kuwa mambo mengi makubwa tayari yamefanyika Kisarawe chini ya uongozi wa CCM na kwamba wananchi wanapaswa kuyaendeleza kwa kura za ndiyo ifikapo Oktoba 29, 2025.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!