Home Kitaifa DKT SAMIA KUPIGA KURA KWA MARA YA KWANZA JIJINI DODOMA ,UCHAGUZI MKUU...

DKT SAMIA KUPIGA KURA KWA MARA YA KWANZA JIJINI DODOMA ,UCHAGUZI MKUU 2025.

Na Deborah Lemmubi-Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa Wito kwa Watanzania wote kujitokeza ili kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari la kudumu la mpiga kura ili kutimiza wajibu wao Kikatiba wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2025.

Dkt.Samia amesema hayo mara baada ya kuboresha Taarifa zake kwenye Daftari la kudumu la Mpiga kura katika Ofisi Serikali ya Mtaa wa Sokoine Kijiji cha Chamwino kilichopo Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma leo Mei 17,2025 ambapo pia amesema kwa mara ya kwanza atapiga kura Makao Mkuu ya Nchi ndomaana amekuja kuboresha Taarifa kwani hapo awali alipokuwa Makamu wa Rais alikuwa akipiga kura Visiwani Zanzibar.

Akiongelea athari za kutokujiandiksha katika Daftari hilo amesema kuwa kwa kutojitokeza na kujiandikisha ni kukataa mwenyewe haki yako ya kikatiba na kupoteza fursa ya kumchagu kiongozi unayemtaka na kulalamika pindi waliojiandikisha watakapochagua kiongozi wanayemtaka.

Niwaombe sana Wananchi wote mjitokeze sana tuje tujiandikishe ili tupate haki ya kupiga kura kwa kutimiza wajibu wetu Kikatiba“.

Aidha ameongeza kuwa serikali imeweka mipango mizuri ambayo itawezesha kila mwenye haki na sifa ya kujiandikisha atajiandikisha.

Hii ni awamu ya pili ya uboreshaji wa taarifa katika Daftari la kudumu la mpiga kura na kujiandika kwa wale ambao wametimiza vigezo na sifa za kupiga kura Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!