Home Kitaifa DC NYANGASA ARIDHISHWA NA EMD NA JENGO LA UTAWALA KISARAWE

DC NYANGASA ARIDHISHWA NA EMD NA JENGO LA UTAWALA KISARAWE

KISARAWE-Pwani

Mkuu wa wilaya ya kisarawe Mhe Fatma A.Nyangasa leo tarehe 02/03/2023 amefanya ziara ya kutembelea miradi miwili ya maendeleo katika wilaya hiyo ikiwemo jengo la wagonjwa la dharura (Emergency Medical Department) pamoja na jengo la utawala.

Ambapo katika ziara hiyo mkuu wa wilaya ameridhishwa na utekelezwaji wa miradi hiyo ya maendeleo na kuipongeza ofisi ya mkurugenzi kwa kazi nzuri inayofanya katika usimamizi wa miradi hiyo.

Mbali na hivyo mkuu wa wilaya amewaagiza viongozi wa halmashauri kuendelea kuwasimamia kwa karibu wakandarasi ili waweze kukamilisha miradi hiyo kwa wakati kwa manufaa ya wananchi na pia kama njia ya moja wapo ya kuunga mkono juhudi za serikali inayo ongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo wananchi

“Naomba tuzingatie ubora wa kazi tunayo Fanya ili tuweze kuzindua miradi iliyo kamilika kikamilifu na pia kama kuna changamoto yoyote katika utekelezaji wa miradi basi tusisite kuwa siliana kwa karibu ili tupate ufumbuzi wa changamoto hizo lakini kubwa Zaidi niwashukuru na kuwapongeza viongozi wote kwa usimamizi mzuri wa miradi hii ya maendeleo” Amesisitiza mkuu wa Wilaya Nyangasa

Nae Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya Kisarawe alishukuru Kwa Niaba ya Watalaam wake Katika Kuupokea na kusimamia Yote ambayo Mhe Mkuu wa Wilaya ameshauri na Yapo Katika Mamlaka yake kiutawala kuyafanyia Kazi,

Mhe Mkuu wa Wilaya Nimeyapokea Yote na Nakuahidi Sisi na Timu yangu Tutayafanyia Kazi Kwa Vitendo na wakati ili Wananchi na Watumishi wapate Huduma Kama Ilivyokusudiwa na Mhe Rais Dr Samia Kwa Kisarawe” alimalizia Peter Ngusa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!