Home Kitaifa CHALAMILA ATOA ONYO KALI KABLA YA KESI YA TUNDU LISSU APRILI 24

CHALAMILA ATOA ONYO KALI KABLA YA KESI YA TUNDU LISSU APRILI 24

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ametoa onyo dhidi ya watu wanaopanga kuanzisha vurugu au kuhamasisha machafuko ifikapo Aprili 24, 2025 siku ambayo Tundu Lissu anatarajiwa kufikishwa mahakamani.

Chalamila ametoa onyo hilo wakati akizingumza na waandishi wa habari Aprili 23,2025 amesema tayari wapo watu wanaowasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya siku hiyo, akisisitiza kuwa vyombo vya dola vitachukua hatua kali za kisheria kwa yeyote atakayejaribu kuvuruga amani au kupuuza mamlaka halali.

Wapo wanaoendeleza mizaha kwa lengo la kutafuta huruma kutoka mataifa ya ndani na nje. Serikali haipo tayari kuona mtu au kundi lolote likikiuka sheria kwa kisingizio chochote,” amesema Chalamila.

Aidha, amesisitiza kuwa viongozi au wananchi wanaokiuka sheria hawatavumiliwa na watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria za nchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!