Home Kitaifa BI. EDITH BAKARI: KILA MWAKA WATOTO 14,000 HUZALIWA NA SIKOSELİ TANZANIA

BI. EDITH BAKARI: KILA MWAKA WATOTO 14,000 HUZALIWA NA SIKOSELİ TANZANIA

Serikali kupitia Wizara ya Afya imeeleza kuwa tayari huduma za uchunguzi wa ugonjwa wa Sikoseli zimesambazwa katika hospitali za mikoa yote, huku hatua zikiendelea kuhakikisha huduma hizo zinapatikana katika Hospitali za Mkoa,wilaya na baadhi ya vituo vya afya.

Hayo yamesemwa leo Septemba 30, 2025 na Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Magonjwa Yasiyo ya Kuambukizwa, Bi. Edith Bakari katika kilele Cha maadhimisho ya mwezi wa kuelewesha jamii juu ya ugonjwa wa sikoseli yaliyo fanyika katika ukumbi wa Shirika la Tumbi (Bertil Melin ) huku yakiwa na lengo la kuongeza ufahamu kuhusu ugonjwa huo.

Aidha amesema takwimu zinaonyesha kuwa kila mwaka Tanzania huzaliwa watoto takribani 14,000 wenye sikoseli na kusema kuwa hii ni changamoto kubwa huku akieleza endapo watu wakipima mapema na kutoa huduma sahihi bado wana nafasi ya kupunguza tatizo hili kwa kiwango kikubwa.

Bi. Bakari amesisitiza upimaji wa mapema kwa watoto pindi wanapozaliwa huku akiwataka vijana kujitokeza kwa wingi kupima vinasaba kabla ya kuanzisha familia na kusema kuwa itawasaidia kufahamu hali zao mapema na kufanya maamuzi sahihi pindi wanapotafuta wenza wa kuanzisha safari ya ndoa na kwakufanya hivyo watakuwa wamekata mnyororo wa ugonjwa wa Sikoseli.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Dr. Kusirye Ukio, amesema wataimarisha huduma za uchunguzi na kuhakikisha dawa za wagonjwa wa sikoseli zinapatikana kwa wakati.

Akitaja idadi ya watu waliojitokeza kufanya uchunguzi kwa mwezi wa huu wa uhamasishaji Dkt Pius amesema zaidi ya wagonjwa 30 walifanya vipimo na wagonjwa 15 waligundulika kuwa ugonjwa huo.

Pia ametoa hamasa kwa jamii kuendela kupima hata mara baada ya kutamatika kwa maadhimisho hayo.

Naye shujaa wa Sikoseli Arafa Said alie hudhuria maadhimisho hayo ameiomba Serikali kupunguza gharama za dawa ili kuongeza upatikanaji wake ili kuwasaidia wagonjwa hao waweze kutumia pia aliwaomba wazazi wenye watoto wa sikoseli wasikate tamaa kuwapeleka shuleni watoto wenye ugonjwa huo kwani na wao wana haki ya kupata elimu kutokana na changamoto zote za kuumwa mara kwa mara.

Maadhimisho hayo Kitaifa yamefanyika Mkoani kwani na hudhuriwa na Viongozi mbalimbali , taasisi na wadau wa maendeleo wakiwemo Hospitali ya Tumbi, Neema Foundation na mashirika mengine yanayoshirikiana na serikali katika kusambaza elimu na kuhamasisha uchangiaji damu kwa wagonjwa wa sikoseli.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!